News Details

Images
Images
  • News

Air France yarejesha Safari zake nchini baada ya miaka 28.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa ameongoza mapokezi ya Ndege aina ya Boeing 787-9 ya Shirika la Air France lililoanza safari nchini kupitia Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ikiwa ni baada ya takribani miaka 28 tangu lilipositisha safari zake nchini mnamo mwaka 1995.

Ujio wa Ndege hii ni matunda ya juhudi za dhati zinazofanywa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kujenga na kuimarisha uchumi wa nchi yetu hususani katika Sekta ya Usafiri wa Anga.

Na pia kuimarika kwa miundombinu katika Usafiri wa Anga nchini inayoendana na kasi ya teknolojia.

Maamuzi ya kurudi kwa Shirika la Air France na kuanzisha safari katika Kiwanja cha JNIA, sio tu yatatoa nafasi kwa abiria kuweza kuchagua na kunufaika na usafiri wa moja kwa moja kutoka Dar es Salaam mpaka Paris, bali pia yataongeza tija na manufaa katika Nyanja za Utalii, biashara, na ajira na hivyo kukuza uchumi kwa nchi zote mbili.