News Details

Images
Images
  • News

BARAZA LA WAFANYAKAZI LA TCAA 2024 LAFANYIKA DAR ES SALAAM

Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wamehimizwa kujitokeza kwa wingi na kutumia fursa yao ya kidemokrasia ya kupiga Kura ili kuchagua viongozi wa serikali za mitaa siku ya Novemba 27,2024.

Wito huo umetolewa  na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Salim Msangi wakati wa akifungua Baraza la wafanyakazi la TCAA lililofanyika Novemba 14, 2024 jijini Dar es Saalaam.

Katika ufunguzi huo Mkurugenzi Mkuu Msangi, pia amewamepongeza Watumishi wa TCAA kwa kuendelea kufanya vikao vya Baraza la Wafanyakazi vyenye tija vinavyoendelea kuwa chachu ya maamuzi makubwa ya kuboresha uboreshwaji wa huduma za Usafiri wa Anga nchini.

Bw. Msangi  ameongeza kuwa,  kufanyika kwa vikao hivyo vya Baraza ni kuimarisha demokrasia mahala pa kazi,na kuwataka wajumbe wa Baraza hilo kurudisha mrejesho kwa watumishi wenzao na kuwahimiza  kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuendelea kutenda kazi kwa ufanisi. 

"Menejimenti inatambua mchango wa kila mtumishi kwa taasisi na ni vyema kila mmoja akatambua kuwa TCAA inajengwa kwa kuanzia na wewe, hivyo nawasihi sana tufanye kazi kwa kushirikiana  na inapobidi msaidie mwingine ili kuhakikisha malengo ya taasisi na ya serikali kwa ujumla yanafikiwa na huduma bora inatolewa" amesema Bw. Msangi.

Mbali na majadiliano, wajumbe wa baraza pia walipata fursa ya kusikiliza wasilisho kuhusu akili ya kihisia “Emotional Intelligence” kutoka kwa Dkt. John Masoyi.