News Details

Images
Images
  • News

TCAA YATOA ELIMU KATIKA MKUTANO WA 8 WA JUKWAA LA WAHARIRI

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi amewasilisha mada kuhusu  utendaji kazi wa TCAA katika Mkutano wa 8 wa mwaka wa Jukwaa la Wahiriri Tanzania (TEF),unaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 06- 09, 2024 katika ukumbi wa NSSF Mafao House- Ilala.

Katika mada hiyo  wahariri walipata fursa ya kuyafahamu kwa kina majukumu ya TCAA. Na pia walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali ambayo yalijibiwa  na Mkurugenzi Mkuu pamoja na wataalam wa Mamlaka walioambatana naye.

Zoezi hilo la TCAA ni sehemu ya mikakati yake ya kutoa elimu kwa wadau wakuu wa vyombo vya habari inalolifanya kila mwaka.

Huu ni muendelezo wa TCAA kuutambua na kukuza ushirikiano na vyombo vya habari ambao ni wadau muhimu katika sekta ya Usafiri wa Anga nchini.