News Details

Images
Images
  • News

WADAU WA USAFIRI WA ANGA WAKUTANA KUJADILI MABORSHO YA KANUNI

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imekutanisha wadau wa sekta hiyo kujadili mabadiliko na maboresho  ya sheria za Usafiri wa Anga nchini.

Akifungua mkutano huo wa siku tatu unaofanyika katika makao makuu ya ofisi za TCAA Banana - Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Salim Msangi amesema huu ni mkutano muhimu sana kwani maoni ya kila mdau yanahitajika katika kuimarisha sekta ya Usafiri wa Anga hapa nchini.

Mkutano huo unaofanyika kuanzia Novemba 6 hadi 8, 2024 unatarajiwa kukusanya maoni yatakayoboresha sheria na kanuni za Usafiri wa Anga nchini.