Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imetia saini Hati ya Makubaliano (Memorandum of Understanding – MoU) kati ya TCAA na Kamandi ya Anga. Utiaji saini huo umefanyika Agosti 10, 2026 jijini Dar es Salaam.
Hati hiyo ya Makubaliano inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya TCAA na Kamandi ya Anga, hususani katika utafutaji na uokoaji (Search and Rescue – SAR).
Ushirikiano huo unatarajiwa kuimarisha uratibu na uwezo wa pande zote mbili katika kutekeleza majukumu yanayohusiana na usalama wa anga.
Katika hafla hiyo Mamlaka ya Usafiri wa anga iliongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dkt Jabiri Bakari akishuhudiwa na Mkurugenzi wa Sheria Bi. Maria Memba na upande wa Kamandi ya Anga iliongozwa na Meja Jenerali Shabani Baraghashi Mani akishuhudiwa na Meja Haika Haule.
Utiaji saini huo unaimarisha ushirikiano wa kitaasisi na ufanisi katika usalama wa anga, sambamba na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayolenga kuimarisha na kukuza sekta ya usafiri wa anga.