TAARIFA KWA UMMA

 

 

 

TAARIFA KWA UMMA

 

USAJILI NA UHUISHAJI WA LESENI ZA VIWANJA VYA NDEGE KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

 

Taarifa hii inatolewa kuwajulisha na kuwakumbusha waendeshaji wa viwanja vya ndege  katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu jukumu la kusajili na kupata leseni za uendeshaji wa viwanja vya ndege kwa mujibu wa Kanuni za Usafiri wa Anga (Viwanja vya ndege) za mwaka 2017.

 

 

Kanuni za Usafiri wa Anga (Viwanja vya ndege) za mwaka 2017 zinakataza uendeshaji wa viwanja vya ndege bila ya kupata usajili au leseni inayotolewa na Mamlaka na ni kosa kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.

 

Waendeshaji wa viwanja vya ndege wanakumbushwa kuwa kuendesha kiwanja bila ya leseni ya uendeshaji au usajili uliotolewa na Mamlaka hii ni kuvunja sheria. Mkurugenzi Mkuu atachukua hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kukataza matumizi ya viwanja visivyosajiliwa.

 

Katika hali hii, waendeshaji wote wa viwanja vya ndege wanapewa hadi tarehe 31 Desemba 2019 kutimiza matakwa ya  sehemu ya III, sehemu ya IV na sehemu ya V ya Kanuni za Usafiri wa Anga (Viwanja vya ndege) ya mwaka 2017. Waendeshaji  wa viwanja vya ndege wasiokuwa na leseni hai wanatakiwa  kuwasilisha maombi yao kwa mamlaka kabla ya tarehe hiyo.

 

Fomu ya maombi pamoja na nyaraka nyingine za mwongozo zinaweza kupatikana kutoka kwa mamlaka kwa kupitia anuani iliyo hapo chini au kupakuliwa kutoka katika tovuti ya mamlaka www.tcaa.go.tz

 

 

 

Mkurugenzi Mkuu,

Mamlaka ya Usafiri wa Anga,

S.L.P 2819

Dar es salaam

Simu: +255222198196

Tovuti: www.tcaa.go.tz

Barua pepe:tcaa@tcaa.go.tz