TAARIFA KWA UMMA

MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA

 

 

 

DAR ES SALAAM                                                                                                                                MARCHI 10, 2019

 

TAARIFA KWA UMMA

SALAMU ZA RAMBI RAMBI KUFUATIA AJALI YA NDEGE YA SHIRIKA LA ETHIOPIA, MACHI 10, 2019

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya ajali ya ndege ya shirika la Ethiopia namba ET 302 ilitoyotokea asubuhi ya tarehe 10 Machi 2019. Ajali hiyo imetokea wakati ndege hiyo ikifanya safari kutoka uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bole kwenda Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi Kenya.

Ndege hiyo aina ya Boeing 737-800 MAX ilipoteza mawasiliano na kituo cha kuongoza ndege cha Mamlaka ya Usafiri wa Anga Ethiopia, dakika sita baada ya kuruka.

Salamu za rambirambi ziende kwa familia za abiria na wafanyakazi wa ndege waliopoteza maisha. Ajali hii ya kusikitisha imeathiri jumuiya yote ya wana usafiri wa anga duniani. Tunasubiri majibu ya ki uchunguzi ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.

 

Hamza S. Johari

Mkurugenzi Mkuu