MNADA WA HADHARA

MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA (TCAA)

 

 

 

MNADA WA HADHARA

                          Tarehe: 28 Mei 2018

  1. Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) inategemea kuondosha Magari yake matano (05) na Bajaj moja (01) kwa njia ya Mnada wa hadhara. Magari hayo na Bajaj yatauzwa kama yalivyo na Mamlaka haitakuwa na jukumu lolote baada ya Mnada.
  2. Minada itafanyika eneo la Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA),Aviation House,Dar Es Salaam na Uwanja wa Ndege Arusha siku ya Jumamosi,tarehe   23 Juni 2018 kuanzia saa nne (4) asubuhi.
  3. Magari yanaweza kukaguliwa na yeyote atakayependa kushiriki muda wa kazi kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa tisa alasiri (3:00-9:00) siku mbili kabla ya mnada(Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Aviation House,Dar es Salaam na Uwanja wa Ndege Arusha)
  4. Orodha ya magari na bajaj yatakayoondoshwa kwa njia ya mnada ni kama ifuatavyo:

Na.

AINA

MWAKA

NAMBA YA CHASSIS

IDADI

MAHALI

1.

Pajero Station Wagon

2003

JMYLNV76W4JOOO851

01

Uwanja wa Ndege Arusha

2.

Land Cruiser Station Wagon

2003

JTECB01J30-1012888

01

Mamlaka ya Usafiri wa Anga

3.

Land Cruiser Station Wagon

2002

JTECB01J60-1000850

01

Mamlaka ya Usafiri wa Anga

4.

Suzuki Grand Vitara

2004

JSAJITTD54V00107607

01

Mamlaka ya Usafiri wa Anga

5.

Nissan Hardbody Pick-up

2006

ADNJ820000E000326

01

Mamlaka ya Usafiri wa Anga

6.

Bajaj

2002

24FBJJ93237

01

Mamlaka ya Usafiri wa Anga

 

MASHARTI YA MNADA

a)    Atakayeshinda mnada atatakiwa kulipa fedha taslimu (hairudishwi) asilimia ishirini na tano (25%) ya bei ya kununulia gari siku ya mnada. Kiasi kilichobakia cha asilimia sabini na tano (75%) ni lazima kilipwe ndani ya siku kumi na nne (14) baada ya mnada.

b)    Mtu yeyote atakayetangazwa kuwa mshindi na akashindwa kulipa asilimia ishirini na tano (25%) ya bei ya gari siku ya mnada atachukuliwa kuwa anavuruga utaratibu wa mnada na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

c)    Mshindi wa mnada atakuwa na jukumu la kufanya malipo yote ya tozo na kodi kuhusiana na gari au bajaj.

d)    Atakayeshinda ataruhusiwa kuchukua gari au bajaj kutoka maeneo ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) au Uwanja wa Ndege Arusha baada ya kukamilisha malipo yote pamoja na tozo na kodi husika.

 

LIMETOLEWA NA:

MKURUGENZI MKUU,